BAADA ya Supastaa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz kuingia kwenye rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki, kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye mradi maalumu uitwao ‘Global Spin’ ulioandaliwa na waandaaji wa tuzo kubwa duniani za Grammy, msanii H Baba ameamua kuvunja ukimya na kumpongeza Diamond.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa H Baba ambaye amekuwa akimponda Diamond na WCB kwa ujumla, ameposti video yake na kuandika; “Mnatakiwa mjifunze mimi ninamaisha yangu binafsi nimeridhika nayo sina ninacho nichakwangu sijashawishiwia namtu yoyote KUMPOST Simbaaa @diamondplatnumz ni mimi mwenyewe nakihelehele changu.
“Kama anafanya poa kwanini nisimpost waswahili wanasema maneno kibao narudia MSUKUMA hanunuliwi wala hanunuliki ata sikumoja mimi sio muajiliwa wa mtu ni mwanamuziki pia nishabiki kama mwanamuziki mwenzangu kaupiga mwingi nisiseme nasema kwa hili @diamondplatnumz kaupiga Mwingi…
“Umeuwaaaaaah ATI nini Ameuwaaaah ATI niniiii Ameuwaaaaah jeshi la mtu mmoja ndio mimi #rais wa insta ndio mimi @h.baba_ wengine fake fake kosa langu ni kihelehele changu mwenyewe page ni yakwangu sipangiwiiiiiiii. mimi sio chawa mimi nishabiki mkubwa nikikubali nimekukubali kutoka moyoni najitoa kufa au kupona.”
Katika post nyingine, H Baba ameposti video ya Diamond na kuandika; “Samahani ndugu zangu hii imejipost yenyewe sijui kunanini hii HUAWEI nilionayo sielewi mwenye ushabiki wa kweli na mimi aninunulie simu.
“Napata tabu kweli kupost hii simu nimeazima tuu simu yangu imedondoka kwenye maji nimeanika juani sijui itapona ngoja nisubiri na mvua zinanyesha sintakuwa hewani mpaka nitakapo pata simu ssanteni mashabiki wa muziki mzuri…”
Diamond ametumbuiza kupitia Virtual concert iliyorushwa Februari 7, 2022. Global Spin ni sehemu ya hafla maalumu iliyoanzishwa mnamo mwaka 2021, kwa lengo la kuutangaza muziki wa Afro Beat, K pop, pamoja na muziki wa Latin ili kuusogeza kwenye ramani ya muziki wa dunia.
Kwenye onesho hilo Diamond Platnumz ametumbuiza wimbo wake mpya ‘Gidi ambao bado hajautoa rasmi, huku miongoni mwa vivutio vikubwa ikiwa ni mpangilio wa namna wahusika wote kwenye onesho hilo walivyokaa na kunakshiwa na mandhari nzuri aliyoiandaa.