KAMPUNI YA MDUNDO YAONGEZA WASIKILIZAJI MILIONI 20 ROBO MWAKA

HUDUMA ya Kusikiliza Muziki Mtandaoni (Mdundo) yaongeza watumiaji kwa 22% barani  Afrika. Muziki wa Kiafrika unalenga kujisimika na kujiimarisha zaidi barani Afrika Jumla ya watumiaji milioni 20 kwa robo mwaka baada ya Q4 ya 2021 kutoka milioni16.3m ya Q3*Yafanya kazi na wasanii zaidi ya 100,000

 Huduma ya utiririshaji wa Muziki wa Kiafrika, Mdundo, imetangaza ukuaji kwa asilimia 22 kwa watumiaji wake kwenye nusu ya mwisho ya 2021. 

Jukwaa hilo lilirekodi watumiaji milioni 20 mwishoni mwa Q4, ikipanda kutoka watumiaji milioni 16.3, kwenye Q3, ikichangiwa na uhitaji mkubwa wa huduma ya muziki iliyo rahisi kutumia, pamoja na upanuzi mkubwa katika maeneo mapya barani Afrika.

Kampuni inaona ukuaji huu endelevu umechangiwa na ushirika wenye nguvu kati yake na kampuni za mawasiliano pamoja na chapa zinazoongoza kwa walaji kama MTN Nigeria, Vodacom Tanzania, Guinness, SportPesa na Standard Chartered Bank, hivyo kushuhudia huduma hii ikiongeza watumiaji wake kwa wingi, soko la kipato cha kati, hasa kati ya eneo la umri wa miaka 18-24.

“Tumebaini ongezeko la uhitaji wa huduma ya muziki inayotolewa mtandaoni, hasa miongoni mwa kundi la watumiaji vijana, walaji wanaofuatilia kikamilifu kuona bidhaa mpya na suluhu za kuunga mkono mfumo wao wa maisha,” amesema Rachel Karamu, Mkuu wa Mdundo.

Ongezeko lililoonekana dhahiri lilirekodiwa Tanzania, Nigeria na Kenya, ikichochewa na kuongezeka kwa umaarufu wa jukwaa hilo, hasa miongoni mwa kundi la umri kati ya miaka 18-24.

Jumla ya watumiaji wa kipekee Q4 kwenye masoko hayo matatu sasa wanafikia milioni 12.1; Tanzania ikiwa na milioni 3.7, Kenya milioni 4 na Nigeria milioni 4.4. masoko mengine makubwa kwa Mdundo ni pamoja na Uganda (milioni 1.8) na Ghana (milioni 1.6). 

Kwa Mdundo kwa sasa inajivunia kuwa na watumiaji milioni 13.3 kwa mwezi kwenye bara lote la Afrika.Mdundo inatazamia ukuaji endelevu zaidi kupitia ubunifu unaolenga kuvutia watumiaji wapya, wakati ambapo masoko ya walaji yanaanza kurejea kwenye hali ya kawaida baada ya kuathiriwa kwa muda mrefu na janga la Covid-19.

“Mwaka 2022 tulitoa maotoeo juu ya ukuaji endelevu wakati tukibuni, si tu katika kupata watumiaji wapya, lakini pia kkwa ajili ya kuweka jukwaa lenye ufanisi kwa washirika wetu wa matangazo ya biashara. 

Katika mazingira yaliyopo, hii inamaanisha kushusha gharama za kufikia chapa za washirika wetu barani,” anasema Karanu.

Anaongeza kwamba Mdundo ina umakini mkubwa kwenye upanuzi ndani ya bara la Afrika.

 “Afrika ina uwezo mkubwa kutokana na ukuaji wa haraka wa soko la kipato cha kati na Tunafanya kazi katika nchi zote za Afrika, na masoko yetu makuu ya kibiashara yakiwa Kenya, Tanzania na Nigeria, tunatazamia kupanua masilahi yetu ya kibiashara hadi Ghana na Uganda mnamo 2022."

Ikiwa imezinduliwa mwaka 2013, Mdundo ni huduma ya muziki mtandaoni ni msingi wa mtandao wa rununu inayowezesha watu kupakua bure mamilioni ya nyimbo kutoka Afrika na sehemu nyingine duniani. 

Watumiaji wa jukwaa hili wanaweza kupakua na kutiririsha muziki kihalali kutoka wavuti ya Mdundo na Android bure na imejumuishwa katika mfumo unaokua wa utangazaji wa kidijiti unaojumuisha baadhi ya chapa kuu duniani za masoko.

Jukwaa hili hufanya kazi na zaidi ya wasanii 100,000 kutoka sehemu mbalimbali barani na pia baadhi ya lebo kubwa kabisa za kurekodi.

 Pia inatetea matumizi halali ya muziki na imekuwa muhimu katika kukomesha upakuaji haramu wa muziki kwenye majukwaa ya mtandaoni.

Mdundo pia hutoa chapa zinazoongoza za watumiaji mbinu ya kipekee na inayofaa kitamaduni ya masoko inayolenga kujenga uaminifu na kukuza mauzo. 

Wateja wake wakuu ni pamoja na chapa kubwa kote Afrika zikijumuisha; Coca-Cola, Standard Chartered, Safaricom, KCB Bank, Kenya Breweries Limited, Serengeti Breweries Limited, Tanzania Breweries Limited, Guinness Nigeria na Nivea.

Watu wanapenda muziki. Ndiyo maana tunaamini kwamba muziki ndiyo njia yenye nguvu zaidi ya kuwasiliana na watu kwa kiwango cha kihisia.

" Kampeni zetu za matangazo ya sauti hutolewa sambamba na muziki kutoka kwa wanamuziki wakuu kuunda ujumbe wa kuaminiana na wa kibinafsi unaoathiri maamuzi halisi ya wateja,” anafafanua Karanu.

Kulingana na utafiti wa 2017 wa PwC, asilimia 38 ya watumiaji milioni 300 wa simu mahiri barani Afrika husikiliza muziki kwenye simu zao kila mwezi. 

Ukuaji wa biashara ya mtandaoni unatarajiwa kukuza matumizi ya muziki, filamu na masuluhisho mengine ya burudani kwa kutumia simu mahiri.Mdundo iliorodhesha hisa zake kwenye Soko la Nasdaq First North Growth Market Denmark mnamo Septemba 2020 na kukusanya $ 6.4 milioni kufadhili upanuzi kote Afrika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii