Waasi wa M23 waripotiwa kuelekea kuunda mfumo wao wa fedha

Ni miezi miwili sasa tangu pale Jiji la Goma lianguke mikononi mwa kundi la waasi la AFC/M23. Tangu wakati huo, benki zote za biashara zimefungwa kwa maagizo ya mamlaka mjini Kinshasa. Kutokana na hali hiyo, katika jiji hili lenye wakazi zaidi ya milioni moja, madawati ya fedha hayafikiki, fedha za kigeni ni chache na uchumi wa ndani umeyumba sana.

Wakikabiliwa na hali hii, baadhi ya waendeshaji uchumi wanafanikiwa kutoa pesa kupitia Kiotamotela ama ATM zilizo nje ya nchi, haswa katika nchi jirani ya Rwanda.

Licha ya baadhi kufaanikiwa kutoa pesa kwa kutumia Kiotamotela maharufu kama ATM za Rwanda, wengine pia hutumia njia za kielektroniki za uhamishaji. Lakini shughuli za kawaida za kila siku kama vile kuweka au kutoa pesa kwenye matawi haziwezekani tena.

Ni katika muktadha huo ambapo AFC/M23 inataka kuunda mfumo wake wa kifedha unaoitwa “Mamlaka ya Udhibiti wa Sekta ya Uchumi, Fedha na Bima”.muundo huu tayari umeundwa kwenye karatasi.

Inatarajiwa kutekeleza jukumu la benki kuu katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa AFC/M23.

Vuguvugu la kisiasa na kijeshi linaloungwa mkono na Kigali pia linataka kuanzisha upya Cadeco, taasisi ya fedha ya umma ya Kongo, inayozingatiwa na wataalamu kadhaa kuwa karibu imesimama.

Uasi huo uliteua usimamizi sambamba, kwa lengo la kuifanya benki kuu katika eneo lililo chini ya udhibiti wake. Mapato ya ushuru yanayokusanywa na utawala wa AFC/M23 yanapaswa kulipwa ndani yake.

Maagizo yalitolewa kwa wabadilisha fedha na waendeshaji uchumi wa ndani kufungua akaunti ndani ya muundo huu. Lakini mfumo huu unakabiliwa na vikwazo vingi, kulingana na wataalam waliowasiliana na RFI, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uhusiano na benki za kimataifa na vikwazo kutoka kwa, shirika la kimataifa ambalo linapigana na fedha chafu.

Kwa upande wake, AFC/M23 inapanga kutegemea nchi jirani, hasa Kenya, Rwanda na Uganda. Je, mradi huu unaenda kutekelezeka  kweli? Kila kitu kitategemea, anajibu mtaalamu mmoja, juu ya kiwango cha kutengwa kwa kimataifa kwa AFC/M23 na majibu ya nchi na benki za ukanda.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii