Kenya"Tanzania Mjipange Na Matokeo

Baada ya golikipa  wa timu aya Taifa ya Kenya Harambee Stars Patrick Matasi kusimamishwa kwa tuhuma za upangaji wa matokeo, @hoseamchopa ameongea na nyota wa zamani wa Yanga Boniphace Ambani na mgombea wa urais katika klabu kubwa Kenya AC Leopards akiweka wazi changamoto kubwa ni kwenye sheria za kumhukumu mtuhumiwa na sasa wakipambana Bunge litengeneze sheria za kuweza kuwafunga wanaofanya matukio haya yanayoharibu taswira ya michezo.

Hili ni funzo pia kwa soka la Tanzania kwani hivi karibuni Mwenyekiti wa bodi ya klabu ya KMC, Songoro Mnyonge alikiri kuwa wamemsimamisha kiongozi mmoja katika timu yao kwa tuhuma hizi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii