• Jumanne , Aprili 1 , 2025

Rais IbrahimTraoré wa Burkina Faso Akataa Kuongezewa Mshahara

Rais wa Burkina Faso, Kapteni #IbrahimTraoré, mwenye umri wa miaka 37, amekataa ongezeko lolote la mshahara, akisisitiza kujitolea kwake kwa wananchi wa nchi hiyo.

Traoré, ambaye alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi, alitangaza kuwa utajiri wake wote ni shilingi milioni 340 za Kitanzania na ataendelea kupokea mshahara wake wa kawaida kama kapteni wa jeshi.

Uamuzi wake wa kukataa ongezeko la mshahara ni tofauti kubwa na hatua za baadhi ya watangulizi wake, ikiashiria enzi mpya ya uongozi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii