Mkuu wa jeshi la Uganda amedai kwamba ni yeye alimteka mlinzi wa kiongozi wa upinzani Bobi Bobi Wine na kwamba anamtesa kwenye eneo lake na kuegesha magari.
Matamshi ya Muhoozi Kainerugaba yamejiri baada ya chama cha Bobi Wine kusema kwamba mlinzi wa kiongozi wao alikuwa ametoweka.
Uganda imekuwa ikikashifiwa na jamii ya kimataifa kwa kuwateka wanasiasa wa upinzani, wa hivi karibuni akiwa ni Kizza Besigye, ambaye alitekwa mwaka uliopita nchini ambapo kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya uhaini nchini humo.
Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mkuu wa jeshi na mwanawe wa kiume wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa X amethibitisha kumzuia Eddie Mutwe, mliniz wa Bobi Wine.
Aidha ametishia kwamba atameteka Bobi Wine kama alivyofanya kwa mlinzi wake.
Wine, msani wa zamani ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi ameibukia kuwa mpinzani mkubwa wa rais Museveni, ambaye ameongoza Uganda tangu mwaka wa 1986.
Tarehe 27 ya mwezi Aprili, chama cha Bobi Wine, National Unity Platform, kilisema kwamba Mutwe alitekwa na watu wenye silaha ambao walikuwa na mavazi ya wanajeshi maalum katika jeshi la Uganda.
Kando na kuthibitisha kumteka na kumtesa mlinzi huyo wa Bobi Wine, Kainerugaba pia amesema anatarajia kumuondoa nguvu zake za kiume.
Mapema mwaka huu, kiongozi huyo wa jeshi la Uganda alitishia kumkata kichwa Bobi Wine kabla ya baadae kuomba msamaha.