Waziri Bashungwa Atolea Ufafanuzi Kwanini Kesi ya Tundu Lissu Kuendeshwa Mtandaoni "Chade,a Walitaka Kulianzisha"

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Watanzania kuelewa kuwa matumizi ya 'Mahakama Mtandao' wakati mwingine yanafanyika kama sehemu ya mkakati wa vyombo vya ulinzi na usalama kuzuia matukio ya uhalifu na uvunjifu wa amani katika nchi

Akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ilipofanya ziara ya kukagua makasha ya kisasa ya 'Mahakama Mtandao' yanayowezesha usikilizaji wa mashuhuri kwa njia ya kiteknolojia katika Gereza la Isanga -Dodoma, Waziri Bashungwa ametolea mfano wa shauri linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu kuwa ililazimika kuendeshwa kwa njia ya mtandao kufuatia kauli za viongozi wa chama hicho zilizokuwa zinaashiria uvunjifu wa amani

Katika ziara hiyo iliyofanyika, Jumatano Aprili 30.2025 Waziri Bashungwa amenukuliwa akisema:


"Jeshi la Polisi linapokuwa na taarifa za kiiterejensia za wazi na zisizo wazi, kwa mfano maandamano ya CHADEMA, na Watanzania ni mashahidi, viongozi wa CHADEMA walisema waziwazi kwamba wataandamana wakakinukishe, Jeshi linapokuwa na taarifa za kiusalama likashirikiana na Mahakama kutoa haki ile ile kwa kutumia teknolojia ya 'Mahakama Mtandao' ili kuzuia fujo mtaani, naomba Watanzania watuelewe"

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii