Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1.
Rais Dkt. Samia amesema kuwa Nyongeza hii itaanza kutumika Mwezi Julai 2025, itaongeza kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi 370,000 hadi shilingi 500,000.
Akizungumza Katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mkoani Singida Dkt. Samia amesema Wafanyakazi wamekuwa na Mchango Mkubwa katika Kuinua Uchumi wa Nchini na ataendelea Kuboresha Maslahi ya Watumishi hao.