Dabi ya Kariakoo Itapigwa tu Liwalo na Liwe

Yanga SC imerudishwa kamati ya rufaa ya TFF, CAS wamesema Yanga walitakiwa kuanzia Kamati ya rufaa ya TFF kwa mujibu wa kanuni za TFF, Bodi ya ligi (TPLB) na CAS.


CAS wamekubaliana na hoja za TFF na Simba Sports Club ambao ni miongoni mwa walioshitakiwa CAS, CAS hawana mamlaka ya kutaka mechi ya DABI isipangiwe tarehe nyingine.


Rufaa ya Klabu ya Yanga imekataliwa CAS na hivyo ni rasmi wameshindwa rufaa yao ambayo waliipeleka CAS.


Shirikisho la soka TFF na Simba Sports Club wao waliwasilisha hoja zao na CAS wamekubaliana nazo na Yanga SC wanatakiwa waanzie kwenye kamati ya rufaa ya TFF baada ya hapo kama isipopatikama muafaka ndipo waende CAS.


✅TFF waliwakilishwa na wanasheria wawili


✅TPLB waliwakilishwa na mwanasheria mmoja


✅Simba Sports waliwakilishwa na mwanasheria mmoja


❌yanga waliwakilishwa na wanasheria WATANO

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii