Wakenya waliotapeliwa nchini Myanmar wemekwama kwenye mpaka wa Thailand

Zaidi ya Wakenya 60 waliookolewa kutoka mikononi mwa makundi ya matapeli wa mtandaoni nchini Myanmar wamekwama kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Thailand wakiishi katika mazingira mabaya, kulingana na taifa hilo la Afrika Mashariki.

Shughuli hizo za utapeli wa mtandaoni ambazo zimeshamiri kwa miaka kadhaa kutokana na sheria mbovu za mpakani nchini Myanmar, zinawavutia wafanyakazi wa kigeni wanaoahidiwa ajira zenye malipo makubwa.

Lakini wakati wafanyakazi hao wanapowasili nchini Myanmar, matapeli hao wanawashikilia mateka na kuwalazimisha kufanya ulaghai wa mtandaoni.

Chini ya shinikizo la mshirika wake China, Myanmar ilitokomeza baadhi ya mitandao ya matapeli hao, na kuwaachilia karibu wafanyakazi 7,000 kutoka nchi 20.

Wakenya 64 ni miongoni mwa walioachiliwa lakini “hawajavuka mpaka kuingia Thailand ili waweze kurejeshwa nchini mwao”, kitengo cha wizara ya mambo ya nje kinachohusika na Wakenya wa Ugaibuni kilisema Jumatatu katika taarifa kwenye mtandao wa X.

“Hi ni kwa sababu mamlaka ya Thailand haijafungua tena mpaka huo tangu tarehe 12 Februari 2025, wakati wimbi la kwanza la wageni 260, wakiwemo Wakenya 23, lilipokadhibiwa jeshi la Kifalme la Thailand,” wizara hiyo iliongeza.

Matokeo yake ni kwamba, wafanyakazi walioachiliwa wanaendelea kusubiri wakiishi katika kambi za muda kwenye mpaka wa Myanmar katika “mazingira mabaya” wakikabiliwa na ukosefu wa huduma za matibabu, maji safi na umeme, ilisema taarifa ya wizira ya mambo ya nje ya Kenya.

Mamlaka ya Kenya imesema wanatafuta njia mbadala ili warejesha raia wao nyumbani.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii