Maua Sama atachukuliwa na Jay Z au Don Jazzy.

Ukiitaja orodha ya wanamuziki hodari wa kike nchini Tanzania, basi huwezi kuliacha jina la Maua Sama, ambaye siku za hivi karibu zimeibuka tetesi za kuwa pengine nyota huyo wa muziki wa bongo fleva akasainiwa na Mavin Records.

Mavin Records ni miongoni mwa Records Label kubwa nchini Nigeria inayomilikiwa na mtayarishaji mahiri wa muziki Michael Collins Ajereh maarufu Don Jazzy.

Uvumi huo umeenea kwa kasi kufuatia Maua Sama kuonekana kuwa karibu na baadhi ya wasanii walio chini ya Label hiyo kiasi cha kutengeneza taswira ya kuwa pengine yuko mbioni kujiunga na familia ya Don Jazzy.

“Nina kipaji na hakika najiamini, Label yeyote kubwa Afrika au hata nje ya Afrika inaweza kufanya kazi na mimi sio tu Don Jazzy, inawezekana hata Roc Nation kabisa, unaweza ukakuta Maua Sama nimetua pale Roc Nation kwa Jay Z,” Alisema Maua.

Chochote kinaweza kutokea, mwaka 2022 ni wenye kuhusu baraka, tukae tayari, kitu kikubwa ni kuendelea kusapoti muziki mzuri.” Alisema Maua.

Maua Sama ameyasema hayo ikiwa zimepita siku chache tu, tangu mwanamuziki Dija kutoka nchini Nigeria anayefanya kazi chini ya Mavin Records kutangaza kuwa yuko mbioni kuja Tanzania kwa madai ya kupewa mualiko na Maua Sama, jambo linalochangia kuendelea kuwepo kwa matumaini juu ya tetesi hizo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii