CCM Arusha wagoma kumpigia Kura mgombea wao

Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Viwandani, Kata ya Unga Limited wametishia kutompa kura za “Ndio” mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Mtaa huo kupitia Chama hicho endapo aliyeshinda kura za maoni (Rasuli Mshana) hatawekwa kama Mgombea katika nafasi hiyo katika Uchaguzi wa Serikali za Mtaa, Novemba 27, 2024

Makada hao wameandamana hadi Ofisi za CCM Arusha Mjini kuonesha kutoafikiana na uamuzi na jina la Mshana kukatwa na kupendekezwa jina la Richard Mbwambo

Akizungumzia na Gadi TV kuhusu suala hilo, Katibu wa Siasa Uenezi wa Arusha, Saipulani Ramsey amesema “Chama hiki hakitishiwi, tunafuata Katiba na taratibu za Chama, hii sio mara ya kwanza kushiriki Uchaguzi, Wanachama wetu wanajua taratibu za kufuata juu ya kitu ambacho hakiwaridhishi.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii