Museveni aunga mkono mahusiano ya vyombo vya habari kati ya China na Afrika

Kampeni ya vyombo vya habari inayojulikana kama “Washirika wa Afrika” iliyoandaliwa na China Media Group (CMG) itakuza mahusiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika, na kuimarisha ushirikiano kwa vitendo baina yao, wamesema marais wa nchi za Afrika.

Tukio hilo, limetumika katika kusaidia shughuli kwa ajili ya mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na AFrika (FOCAC), likilenga kuimarisha mabadilishano ya vyombo vya habari na ushirikiano kati ya China na Afrika,

Wakati huo huo tukio hilo likidaiwa kuimarisha mabadilishano ya kiutamaduni na mafunzo ya pamoja katika enzi ya digitali.

Marais kadhaa wa Afrika pia walielezea azma yao ya kuimarisha mabadilishano ya habari kati ya China na Afrika na kuiamrisha ushirikiano kwa vitendo katika ujumbe wao kwa njia ya video katika tukio hilo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema, “Kwa kuwa China ni rafiki wa Afrika. Naunga mkono mkutano wa vyombo vya habari unaofanyika Beijing."

"Nawatuma vijana wetu, nataka nao wahusishwe. Unajua, hakuna kitu ambacho sikijui kuhusu China, na wao wanatufahamu sisi pia, lakini nataka vijana kuungana na nyinyi vijana wenzao.” aliongeza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii