MWANADADA ambaye kwa sasa yuko
kwenye ubora wake katika muziki wa kizazi kipya Zuhura Othman Soud
maarufu kwa jina la Zuchu ameweka wazi kuwa amewahi kutoka 'Out' na Bosi
wake Nasseb Abdull a.k.a Diamond kwa ajili ya kupata Dinner.
Mbali
ya kupata Dinner pamoja amesema amewahi kumpikia chakula nyumbani kwake
lakini ameshindwa kuweka wazi iwapo wawili hao wanatoka kimapenzi.Kila
alipoulizwa Kama ana uhusiano na Diamond ,Zuchu ameshindwa kujibu huku
akibaki kucheka na wakati akisema hapana.
Akizungumza katika
kipindi Cha Mashamsham kilichorushwa leo na Redio ya Wasaf FM, Zuchu
amezungumza mambo mbalimbali kuhusu muziki wake na tasnia ya muziki kwa
ujumla huku akielezea jinsi anavyomfahamu Diamond.
Alipoulizwa
iwapo kuna jambo zito linakuja kati yake na Diamond, Zuchu amesema
hakuna lakini amekiri Anko Shante ambaye ni mume wa mama yake Diamond
amefika nyumbani kwao,ingawa hajui alikwenda kufanya nini."Sijui Kama
nimetolewa mahari,Anko Shante amekwenda nyumbani ,labda kuna mambo yao
walikwenda kuongea maana wale wakubwa.Kuhusu kutolewa mahali ndio
nasikia kwenu."
Watangazaji wa kipindi hicho wakiongozwa na Dida
Shaibu walitaka kufahamu iwapo anataka kuolewa na Diamond Zuchu
alionekana kung'ata maneno lakini watangazaji hao walithitisha kuwa na
uhusiano na alipoulizwa Februari 14 ambayo ni siku ya wapenda nao
amesema atakuwa na mpenzi wake.
Hata hivyo kadri alivyokuwa
akiendelea kuhojiwa Zuchu anaonesha licha ya kutaka kuficha uhusiano
wake lakini haikuwa rahisi kwani watangazaji walikuwa na data zote
kuhusu mahusiano ya Diamond na Zuchu.
Wakati wa kipindi hicho
Mama Dangote pamoja na ndugu zake Diamond walikuwa wakifuatilia
mahojiano ambapo Zuchu alipoulizwa Diamond anapenda chakula gani amejibu
anapenda ndizi na mama Dangote anapenda Pweza.
Hata hivyo kwa
mujibu wa Juma Lokole ambaye naye ni mtangazaji wa kipindi jicho
amethibitisha Diamond amepeleka mahali na barua ya uchmba, barua ya
uchumba imepelekwa na Anko Shamte.
Akiendelea kuzungumza Zuchu
amekiri hakuna jambo lolote ambalo anaweza kulifanya bila kupata idhini
ya Diamond , alipoulizwa anafanya kivyo kama nani akajibu kama Bosi
wake.Alipoulizwa kama yeye anaficha uhusiano wake na Diamond, anatamani
Diamond amuoe nani kati ya Hamisa Mobeto,Zari Hassan na
Tanasha,ameshindwa kujibu swali hilo na kubakia akicheka tu.
Alipoulizwa
kama anamuonaje Diamond katika eneo la mapenzi,amejibu ni mtu mzuri,
anajua kupenda na mtu ambaye si mchoyo,alipotakiwa kueleza amejuaje
akasema anaona kwa wanawake ambao Diamond amekuwa nao(Nimeona kwa Mawifi
zetu).