Ni Mrembo kutokea Afrika Kusini, Ami Faku ambae kwasasa ndie Malkia wa muziki unaofahamika kwa jina la Amapiano.
Ami Faku ni msanii wa siku nyingi ila wengi wameanza kumfuatilia baada ya kusikika kwenye rekodi mbili zilizoachiwa na wakali Kabza De Small & Dj Maphorisa.
Rekodi ambazo zimempa umtambulisho katika muziki wa Amapiano ni Asibe Happy & Abalele ambazo mpaka sasa zinaendelea kupeta katika platfrom mbalimbli.
Sasa Good news ninayotaka kukupatia ni kwamba Staa huyo anatarajiwa kutua Tanzania kuwaimbia mashabiki wa muziki wa Amapiano.
Staa huyo atazinogesha kumbi za starehe ikiwemo Elements Masaki tarehe 5th Jumamosi na tarehe 6th Jumapili Kidimbwi Beach.
Hii ngoma ya kwanza iitwayo Asibe Happy aliyoshirikishwa na wakali Kabza & DJ Maphorisa.