IKIWA ni wiki chache baada ya mtangazaji wa Clouds Media, Meena Ally kuchafuliwa mitandaoni kwa kusambazwa picha ya ngono asiyohusika nayo, hatimaye ameamua kuzungumza namna ambavyo wanawake wengi wa Kitanzania wamekuwa wahanga wa kudhalilishwa mitandaoni.
Kauli hiyo ye Meena inakuja ikiwa ni siku moja baada ya kusambaa kwa Video ya Aristote akimrushia madongo kwa kudai kuwa msanii Wema Sepetu kuwa hana shepe na wala hana gari, maisha yake yamekuwa magumu kiasi cha kulazimika kutumia usafiri wa Uber na Bolt.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meena Ally ameandika; “Moja kati ya tatizo linalokua kwa kasi na hii mitandao Tanzania ni tatizo la Cyber bulling na cyber sexual abuse. Kwa bahati mbaya sana siku hizi watu wana njaa ya kuona mwenzao anadhalilishwa mtandaoni au kufanya kazi hiyo ya udhalilishaji wenyewe.
“Habari zinazofika mitandaoni hazithibitishwi kama inavyotakiwa na udhalilishaji unaomkuta mtu watu wanaushadidia bila kujali anaedhalilishwa atakua anajiskiaje. Kwa bahati mbaya wanawake ndio victims wakubwa sana sana wa hili tatizo maana wao wanaonekana easy target!
“Mtu unashikilia kudhalilisha mtu wakati humjui vizuri na wala hata hujui anakula nini asubuhi na analalaje,ila vidole vyako na smartphone na sometimes camera vinakudanganya kwamba unaweza kumwambia chochote kile.
“Ndugu zangu,mtu yeyote unaemtolea maneno ya kashfa haujui anapitia nini kwenye maisha yake, jitahidi ujiangalie mwenyewe kwanza, kuna watu wanajiua sababu ya cyber abuse, please tusijiskie easy kudhalilisha mtu au kushupalia maneno ya mtandao.
“This is a public call to @polisi.tanzania na mamlaka zote husika, wanawake tunadhalilishwa sana mitandaoni na tunaomba hili jambo mlishupalie kabla halijakua zaidi na zaidi! Pole @wemasepetu you are a sweetheart, its hard to be alive in this generation of coward bullies that are ready to ruin everything someone works hard for. Inshaallah hili litapita