Sugu arejea kwenye muziki

RAPA mkongwe na mmoja wa waasisi wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu, anarejea rasmi kwenye muziki baada ya kuanza mazoezi kwa ajili ya kurejea jukwaani baada ya ukimya mrefu.

Hivi karibuni Sugu ameonekana studio na prodyuza wa Tongwe Records, Bin Laden pamoja na msanii Billnass au Nenga ambapo ngoma yao ipo mbioni kutoka.

“Sitafuti six packs or whatever, ni maandalizi madogo tu ya concert, masaa mawili kwenye stage siyo mchezo…” anasema Sugu kupitia Instagram katika video inayomuonesha akiwa gym.

Kumbukumbu zinaonesha kwamba, Sugu alikuwa Mbunge wa Mbeya-Mjini kwa kipindi cha miaka 10 tangu mwaka 2010 hadi 2020, jambo lilomfanya kuweka muziki pembeni kidogo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii