Harakati ndogo mpakani mwa Rwanda na Uganda baada ya kufunguliwa tena

Kuna harakati kidogo kwenye mpaka wa Gatuna wa Rwanda na Uganda, ambao umefunguliwa tena baada ya karibu miaka mitatu ya kufungwa.

Mpaka huo ulifungwa mwaka 2019 kufuatia mvutano kati ya nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Uganda, ujenzi wa ofisi za forodha - ambazo ni sehemu ya mfumo wa mpaka mmoja unaotekelezwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki - unaendelea.

Kufunguliwa kwa mpaka kulitangazwa wiki iliyopita baada ya mkutano kati ya Rais wa Rwanda Paul Kagame na Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba wa Uganda, ambaye ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni.

Rwanda ilikuwa imeishutumu Uganda kwa kuwazuia na kuwatesa raia wake huku Uganda ikiishutumu Rwanda kwa kupenyeza ujasusi wake wa kijeshi. Nchi zote mbili zilikanusha tuhuma hizo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii