Maandamano ya kupinga ugumu wa maisha yaendelea Iran

Waandamanaji nchini Iran wamepiga kelele na kuandamana hadi Ijumaa asubuhi kuendelea kupinga ugumu wa maisha.

Waandamanaji wa Iran wamepiga kelele na kuandamana mitaani hadi Ijumaa asubuhi baada ya wito uliotolewa na mrithi wa ufalme aliye uhamishoni kuitisha maandamano, licha ya hatua ya utawala wa Iran kukatisha mawasiliano ya intaneti na simu za kimataifa.

Video fupi za mtandaoni zilizosambazwa na wanaharakati zilionekana zikiwaonyesha waandamanaji wakipiga kelele kuipinga serikali ya Iran huku vifusi vya taka vikienea mitaani katika mji mkuu, Tehran, na maeneo mengine. Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimevunja ukimya wake leo Ijumaa kuhusu maandamano hayo, vikidai "mawakala wa kigaidi" wa Marekani na Israeli walichoma moto na kusababisha vurugu. Pia vilisema kulikuwa na "majeruhi," bila kufafanua zaidi.

Kiongozi mkuu wa Iran ⁠Ali ‍Khamenei ametoa hotuba kuhusu vitendo vya kigaidi huku maandamano ya kupinga ugumu wa maisha yakiendelea kote nchini.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii