Urusi yaishambulia Ukraine kwa kombora jipya la Oreshnik

Urusi imesema hivi leo kwamba imetumia kombora jipya chapa Oreshnik pamoja na silaha nyingine katika shambulizi kubwa dhidi ya Ukraine.

Maafisa wa Ukraine wamesema watu wanne wameuawa na wengine wasiopungua 22 wamejeruhiwa katika mji mkuu Kiev usiku kucha. Urusi haikusema kombora la Oreshnik lilipiga wapi, lakini vyombo vya habari vya Urusi na wanablogu wa kijeshi walisema lililenga kituo kikubwa cha kuhifadhi gesi asilia chini ya ardhi katika eneo la magharibi la Ukraine la Lviv.

Jeshi la anga la Ukraine lilisema Urusi ilishambulia Ukraine kwa kutumia ndege zisizo na rubani 242 na makombora 36. Jeshi pia limesema kombora moja la masafa ya kati lilitumika, lakini haikulitaja hili kama kombora la Oreshnik.

Pia liIlisema kombora hili lilirushwa kutoka eneo la majaribio la Kasputin Yar katika eneo la Astrakhan la Urusi, linaloaminika kuwa eneo la kufyatulia makombora ya Oreshnik.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii