Mwanadada mkali wa muziki wa dancehall kutoka nchini Jamaica ambaye amefanikiwa kwa asilimia kubwa kuliteka soko la muziki nchini marekani shanseea ambaye mapaka sasa amefanikiwa kufanya kazi na wasanii wengi kutoka marekani akiwemo,Tyga.
Shenseea ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake akiwa ameshirikiana na Megan stallion ameweka wazi namna ambavyo alikutana na megan na kudai kuwa Megan alimualika katika sherehe hali yakuwa yeye sio mtu wa sharehe lakini aliitikia mualiko ambao pia ulikuwa na mastaa wengi wa marekani.
Lakini shensee ameweka wazi kuwa alishangazwa na megan kuwa ni mtu ambaye anamfatilia na anafatilia mziki wake kitu ambacho hakudhani vilevile alimfata na kumsalimia na kuzungumza mawili matatu na hiyo ilikuwa nafasi nzuri ya wao hata kuamua kufanya wimbo Pamoja ambao unaitwa Lick.