Mkali wa afropop kutoka Nigeria, Skales auanza mwaka 2022 na ‘No body to Somebody’

Msanii Skales kutoka Nigeria ambaye tangu aingie kwenye tasnia Huu ni mwaka wake wa 12 , Skales ameongeza thamani kutoka kuwa Msanii Mdogo Mwenye Kipaji (talanta) mpaka kuwa icon wa afropop na orodha iliyojaa nyimbo nyingi ambazo zinafanya vizuri kwa kasi ya kimataifa

Baada ya kizuizi cha muda mrefu Nigeria kilichotekelezwa na COVID-19, alielekeza nguvu kwenye EP yake “Healing process EP” Yenye mchakato wa uponyaji, tafakari,simulizi Za kufikirisha ambazo hakika zilimpeleka Hadi kwenye kilele cha taaluma yake.

Mwaka 2021 malengo yake makubwa yalikuwa nikurudi kwenye fomu ya kuunda nyimbo za pop ambazo zilimfanya kuwa juu katika Chati nyingi ndani na nje ya Nigeria. Nyimbo kama vile “Kayefi,” ambayo ilihusu dhana ya kupata urafiki wa kimapenzi huku “This Your Body,” wimbo aliomshirikisha Davido ulikuwa ni wimbo wa nadharia ya furaha ya mwili wa mwenzi. Pia , alitoa “I Dey Miss You,” wimbo wa kuchezeka na ulifanya vyema.

Skales 2022 , amekuja na “No body to Somebody” Ukiwa ni wimbo unaohadithia maisha yake na kuwapa Nguvu wale wote wanao tafuta bila mafanikio kuwa iko siku watafikia malengo Yao. Maneno kadhaa kwenye wimbo huu ni ya nyimbo Za injili maarufu miaka ya 80, “Nobody 2 Somebody”

Skales anaelezea namna anavyopitia msururu wa hali ngumu ambazo anawahimiza wasikilizaji wake kuendelea kupigania ndoto zao na kufanya kazi zao ili kufaulu maisha yao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii