NAPE ATOA MAELEKEZO KWA KATIBU MKUU

Waziri wa habari,mwasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt Jimmy Anazi kuhakikisha mameneja wote wa shirika la posta Tanzania wanashirikishwa katika utekelezaji wa mradi wa anuani za makazi ambao serikali imeelekeza ukamilike ifikapo mwezi may mwaka 2022 badala ya mwaka 2025.

Waziri Nape ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano wa 28 wa balaza kuu la wafanya kazi wa shirika la posta nchini,ambapo ameeleza kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha zaidi utendaji kazi wa shirika hilo.

"Sasa nataka turudi jikoni na hapa nimuombe katibu mkuu ebu nenda ukalisimamie hili jambo uhakikishe mameneja wote kutoka kwenye mikoa yote,kwanza wawe wajumbe halali na wakudumu kwenye vile vikao vinavyosimamia jambo hili na yapelekwe maelekezo maalumu kwa sababu hawa ndiyo wenye jambo lao hili jambo ni lenu wengine wafanye kuwasaidieni."Amesema Mh.Nape


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii