Idadi ya watu waliokufa kutokana na dhoruba kali iliyopiga kwenye
nchi tatu za kusini mwa Afrika imeongezeka. Hadi kufikia leo jumla ya
watu 86 wameorodheshwa kuwa wamekufa kutokana na dhoruba hiyo huku
wahudumu katika vitengo vya dharura wakiendelea kukarabati miundombinu
iliyoharibiwa na kuwasaidia maelfu ya watu walioathiriwa na dhoruba
hiyo. Dhoruba Ana ilisababisha mvua kubwa nchini Madagascar mnamo siku
ya Jumatatu kabla ya kupiga katika nchi za Msumbiji na Malawi. Mamlaka
katika nchi hizo tatu bado zinatathmini kiwango kamili cha uharibifu,
wakati kulikuwepo na hofu ya dhoruba nyingine katika Bahari ya Hindi.
Idadi ya vifo vilivyoongezeka ni watu 48 nchini Madagascar, Msumbiji
watu18 na watu 11 nchini Malawi. Dhoruba hiyo imepiga pia nchini
Zimbabwe na hakuna vifo vilivyoripotiwa nchini humo.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii