Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso ameahidi kurejesha
usalama, utulivu na umoja katika nchi hiyo iliyomo katika mgogoro. Hata
hivyo ameonya kuwa usaliti hautavumiliwa na utawala wake mpya. Kiongozi
huyo, LuteniKkanali Paul-Henri Sandaogo Damiba amelihutubia taifa kwa
mara ya kwanza tangu kutwaa mamlaka mapema wiki hii baada ya kumwondoa
madarakani rais Roch Marc Christian Kabore aliyechaguliwa kwa njia ya
kidemokrasia. Kanali Damiba amesema, Burkina Faso inakabiliwa na mgogoro
usiokuwa na kifani na hivyo jukumu la kipaumbele kwa utawala wake wa
kijeshi ni kurejesha usalama, kuimarisha ari ya wanajeshi na kusikiliza
maoni ya wananchi. Kiongozi huyo wa kijeshi pia ameitaka jumuiya ya
kimatifa iiunge mkono nchi yake ili iweze kuanza tena juhudi za kuelekea
kwenye maendeleo. Amesema atarejesha katiba wakati utakapokuwa sawa.
Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS wanakutana
leo kuijadili hali hiyo.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii