Roketi iliyorushwa na kampuni ya uvumbuzi wa anga za juu ya bilionea Elon Musk inakaribia kugonga ndani ya mwezi na kulipuka.
Chombo kinachosaidia roketi kulipuka kwa Falcon 9 kilikwenda katika anga za juu mwaka 2015, lakini baada ya kukamilisha safari yake, hakikuwa na mafuta ya kutosha ya kukirejesha duniania na badala yake kilibakia katika anga za juu
Mtaalamu wa masuala ya anga za juu Jonathan McDowell amesema kuwa itakuwa mara ya kwanza kwa roketi isiyoongozwa kugongana na mwezi. Lakini anasema athari yake itakuwa ndogo.
Roketi hiyo iliachwa katika (muhimili) orbit ya juu miaka saba iliyopita baada ya kukamilisha kazi ya kutuma setilaiti ya hali ya hewa katika safari ya maili milioni.
Ilikuwa ni sehemu ya mpango wa uvumbuzi wa anga za juu wa Bw Musk – SpaceX, ambayo ni kampuni ya kibinafsi ambayo lengo lake kuu ni kuwawezesha binadamu kuishi katika sayari nyingine