Asilimia 95 ya walioumwa Uviko-19 hawakuchanjwa

Serikali imesema watu 3,147 walilazwa hospitalini kutokana na Uviko-19 kati ya Septemba 2021 mpaka Januari 23, 2022 ambapo kati yao 2990 sawa na asilimia 95 walikuwa hawachanja.

Pia, imesema kuwa mpaka sasa ni watu 1,922,019 waliochanja sawa na asilimia 3.3 ya Watanzania waliolengwa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Januari 26, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu baada ya kupokea shehena ya chanjo 800,000 za Sinopharm ambazo ni sawa na dozi 400,000 kutoka Serikali ya watu wa China.

“Wagonjwa waliokuwa mahututi katika vyumba vya uangalizi maalumu kwa siku ya Januari 23 mwaka huu ICU walikuwa 31 kati yao 30 walikuwa hawajachanjwa.

Vifo vilivyotokea vilikua 76 kati ya hivyo vifo 73 viliwahusisha wagonjwa ambao hawakuchanja,” amesema Waziri Ummy.

Amewataka Watanzania kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya kupima kwa kuwa si kila homa au mafua ni Uviko-19

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii