Sam Larry Akamatwa na Police Nigera Kuhusika na Kifo cha Mwanamuziki Mohbad..

Promota Wa Muziki Na Rafiki Wa Karibu Wa Naira Marley #SamLarry Ameripotiwa Kurudi Nchini Nigeria Na Kukamtwa Na Jeshi La Polisi La Lagos. Polisi Wamemkata Sam Larry Kwasababu Ya Uchunguzi Unaondelea Wa Kubaini Chanzo Kilichopelekea Kifo Cha Muimbaji Mohbad

Msemaji Wa Kamanda Wa Polisi Wa Jimbo La Lagos, SP Benjamin Hundeyin Amethibitisha Taarifa Hiyo; "Ndiyo, Balogun Eletu almaarufu Kama Sam Larry sasa yuko chini ya ulinzi wetu. Kwa sasa anasaidia uchunguzi unaoendelea.”

Sababu Nyingine Ya Sam Larry Kusaidia Uchunguzi Wa Kifo Cha Mohbad Ni Kutuhumiwa Kwake Kwa Kuwahi Kushtakiwa Na Mohbad Kwa Kumpiga, Kumtisha Kifo Pamoja Na Kumkosesha Amani Lakini Pia Ndiyo Anadaiwa Kuwa Baba Halali Wa Mtoto Wa Mohbad

Kumbuka Wiki Iliyopita Polisi Walitoa Taarifa Kuwa Uchunguzi Wa Mwili Wa Marehemu Mohbad Umekamilika Na Sasa Wanasubiri Kuyatangaza Matokeo. Pia Muuguzi Aliyemchoma Sindano Mohbad Nae Tayari Alishakamtwa. Kwa Watuhumiwa Wengine Wanaosubiri Kuhojiwa Ni Kama Wale Waliokuwa Nae Siku Aliyofariki, Mke Wake (Wumni) Pamoja Na Naira Marley Ambaye Anahitaji Polisi Wamhakikishie Usalama Wake Ili Arudi Nchini Nigeria Akitokea UK

Mohbad Alifariki Sept 12 Ikorodu Nigeria Baada Ya Kutoka Kwenye Show Na Alizikwa Siku Ya Pili Yake

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii