wachezaji wa klabu ya Singida Big Stars Khalid Aucho amefungiwa michezo mitano (5) na kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 kwa kosa la kufanya kitendo kisicho cha kiuanamichezo dhidi ya Adam Adam wa klabu ya TRA United.
Kutokana na kitendo kilichotokea wakati wa mechi ya hivi karibuni ambapo Aucho alimpiga na kumsukuma Adam Adam katika hatua ambayo iliangaliwa kama ukiukwaji wa Kanuni ya 41:21 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Aidha adhabu hiyo inatolewa ili kulinda utu na heshima ya mchezo wa mpira wa miguu na kuonyesha kuwa vitendo vya ukiukwaji wa sheria haviwezi kubadilika kuwa kawaida.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime