Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Dkt. Seif Shekilaghe, amepongeza maendelo ya mradi wa upanuzi wa jengo
la mama na mtoto na kumtaka mkandarasi kumaliza kazi iliyobakia pamoja
na maboresho kabla ya tarehe 30/04/2022 ili wananchi waanze kulitumia.
Dkt.Shekhalage
ameyasema leo jijini Mbeya wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya
Kanda Mbeya kujionea Hali ya utoaji huduma pamoja na kukagua maendeleo
ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na hospitali hiyo.
Katika
ziara hiyo Dkt. Shekilaghe amepokea taarifa ya hali ya utoaji huduma za
afya na maendeleo ya ujenzi wa mradi wa jengo la mama na mtoto ambao
kwa Sasa umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 92.
Dkt.
Shekilaghe, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea
kushirikiana na vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili kutatua
changamoto mbalimbali zilizopo kwa lengo la kuboresha hali ya utoaji
huduma za matibabu kwa wananchi na kuwasihi watumishi wa afya kudumisha
ushirikiano, nidhamu na maadili ya taaluma zao kazini.
Aidha,
Dkt. Shekilaghe amewataka wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya
kutoa huduma kwa njia ya mkoba (outrich) ili kuwajengea uwezo watoa
huduma waliopo kwenye hospitali ngazi ya mkoa na wilaya kwa ukanda wa
Nyanda za juu Kusini kwa lengo la kuboresha huduma na kupunguza rufaa