Home HABARI MSEMAJI JESHI LA ZIMAMOTO AENDELEA NA ZIARA ZA KUBORESHA UHUSIANO MSEMAJI JESHI LA ZIMAMOTO AENDELEA NA ZIARA ZA KUBORESHA UHUSIANO

MSEMAJI na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi ameendelea na ziara yake kwa ajili ya kujitambulisha, ambapo leo tarehe 25 Januari, 2022 amemtembelea Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime, katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dodoma. 

SACF Nzalayaimisi alipokelewa na mwenyeji wake SACP Misime na kujadili mambo mbali mbali lengo likiwa ni kuboresha uhusiano uliopo baina na taasisi hizi mbili. 

Katika mazungumzo hayo walijadili ni kwa namna gani Askari na Maafisa wanaotekeleza majukumu yao kwenye Vitengo vya Habari kushirikiana na kubadilishana ujuzi katika tasnia hii ya Habari na Elimu kwa Um

Pamoja na ziara hiyo ya kujitambulisha, Msemaji Nzalayaimisi alikutana na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna (DCP) Maria Nzuki na kufanya mazungumzo ambayo waliongelea maswala, umuhimu wa kuweka madawati ya Jinsia na Watoto katika vyombo vya ulinzi na usalama ili kutoa elimu pamoja na kutatua changamoto zinazotokea kwenye jamii.

Pia walizungumzia uboreshaji wa majukumu katika utendaji kazi wa kila siku kwa upande wa Maafisa na Askari Wanawake wanapotekeleza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa bidii kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na sekta nyingine. Katika mazungumzo yao waliwataka wanawake wenzao kuwa bega kwa bega katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili dhidi wanawake na watoto.

Kwa upande wake Msemaji Mpya wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji SACF Puyo Nzalayaimisi, ameshukuru kwa mapokezi mazuri na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha Jamii ya watanzania inakuwa salama nyanja zote za Usalama pamoja na kuokoa Maisha ya watu na mali zao.

ma.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii