NEDY MUSIC :CHRISTIAN BELLA KWANGU NI KAMA KAKA

Alianza kung’ara kupitia muziki wake akiwa kama yeye na baadae kushikwa mkono na Ommy Dimpoz chini ya Pkp ambaye pia alifanikiwa kumuinua kwa kiasi kikubwa sana lakini pia baada ya muda Nedy alitangaza kuachana na Pkp na kuja na Fine boy ambayo ndio brand name ya kampuni yake .

 

Hivi karibuni Nedy music aliachia kazi mpya akiwa amemshirikisha msanii wa muziki wa dansi Christian Bella wimbo uitwao CHINI ambao pia unaendelea kufanya vizuri,vilevile wamewahi kufanya ngoma mikaa miwili nyuma.

 

Kupitia kipindi cha burudani cha HITZONE kupitia Jembe fm Nedy music amehojiwa na kuweka wazi ukaribu wake na Christian Bella na kusema haya:-

“Christian Bella ni kama kaka kwangu kwa sasa yani tumefikia hatua ya familia kabisa lakini pia ni mtu ambaye licha ya kumkubali ni mtu ambaye huwa anasikiliza muziki wangu mara kwa mara kabla sijatoa n ahata kunipa ushauri wa aina tofauti tofauti kimuziki n ahata nje ya muziki”.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii