Hatua hiyo imekuja, miezi miwili baada ya rais Ouattara kuchaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, baada ya kupata ushindi wa karibu asilimia 90 ya kura.
Waziri Mkuu wa Cote Dvoire, Robert Beugré Mambé na serikali yake amejiuzulu, baada ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika Desemba 27 mwaka uliopita.
Jana Jumatano, Januari 7, Rais Allasane Ouattara amekubali kujiuzulu kwa Mawaziri wake na Waziri Mkuu Mambé, licha ya chama chake cha RHDP kushinda uchaguzi huo kwa asilimia 77.
Hatua hiyo imekuja, miezi miwili baada ya rais Ouattara kuchaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, baada ya kupata ushindi wa karibu asilimia 90 ya kura.
Kwa mujibu wa katiba ya Ivory Coast, mawaziri hawaruhusiwi kushikilia nyadhifa za ubunge kwa wakati mmoja. Hadi waziri mkuu mpya na baraza jipya la mawaziri vitakapoteuliwa, mawaziri wanaoondoka wataendelea kushughulikia shughuli za kila siku za serikali.
Rais Outtara sasa anatarajiwa kumtaja Waziri Mkuu mpya na kuwateuwa Mawaziri wapya katika siku zijazo, baada ya chama chake kupata viti 198 kati ya 255 katika bunge la kitaifa.
Ripoti zinasema, huenda baadhi ya Mawaziri waliojizulu wakarejeshwa tena kwa sababu, wamechaguliwa kama wabunge.
Bunge litarejea katika kikao chake tarehe 19 Januari 2026 kwa ajili ya kumchagua Spika mpya, hatua itakayoashiria kuanza kwa mzunguko mpya wa kisiasa nchini humo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime