Afisa wa uhamiaji ampiga risasi mwanamke mwenye umri wa miaka 37

Afisa wa uhamiaji nchini Marekani, amempiga risasi mwanamke mwenye umri wa miaka 37 siku ya Jumatano kwenye mji wa Minneapolis.

Maafisa wa serikali ya rais Donald Trump, wanadai kuwa mwanamke huyo kwa jina la Renee Nicole Good, alilenga kumgonga kwa gari afisa huyo wa uhamiaji.

Aidha, maafisa wa serikali wanasema, kitendo cha kupigwa risasi, ilikuwa ni kujilinda dhidi ya mwanamke huyo.

Hata hivyo, Meya wa Minneapolis Jacob Frey, amemshtumu afisa huyo wa uhamiaji kwa kutumia vibaya silaha, iliyosababisha maafa.

Tukio hili, limetokea wakati idara ya uhamiaji, ikiendeleza msako kwa agizo la rais Trump kuwasaka wahamiaji haramu.

Rais Donald Trump, kupitia ukurasa wake wa kijamii, amesema ni vigumu kuamini kuwa afisa huyo wa uhamiaji bado yupo hai, baada ya kugongwa na gari.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii