Mbunge Segerea, atwishwa kero ya maji Bonyokwa

Mbunge wa Segerea (CHAUMMA), Agnester Lambart, amefanya ziara katika Kata ya Bonyokwa, kusikiliza kero za maji katika eneo hilo.

Miongoni mwa mambo ambayo alikutana nayo katika ziara hiyo ni pamoja na kero za wasomaji wa ankara wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) eneo la Tabata na Kinyerezi.

Wananchi wamelalamikiwa kubambikia wateja Ankara, licha ya kwamba baadhi ya wateja wao hawapati huduma hiyo ya maji kwa muda mrefu.

Nyingine ni lugha chafu ya wasomaji hao wa ankara ambao pia walilalamikiwa kukosa ushirikiano kwa wananchi huhusani pale wanapokwenda kwenye nyumba zao kutoa huduma hiyo.

Baadhi ya wananchi katika kata hiyo wamesema kero ya kukosa maji katika eneo hilo imekuwa sugu, licha ya kulalamika kwa muda mrefu.

Aidan Leonce, ni mmoja wa wananchi wanaoishi katika Mtaa wa Canada katika kata hiyo, amesema tangu mwaka jana, Oktoba hawajapata huduma hiyo ya maji lakini ankara wamekuwa wakipatiwa kila mwezi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii