Mchekeshaji maarufu na mtangazaji wa tv na radio Broderick Stephen Harvey a.k.a Steve Harvey ni moja ya watu wenye ushawishi mkubwa katika sekta ya burudani duniani.
Sasa steve Harvey ambaye inafahamika kuwa binti yake aitwaye Lori Harvey aliye katika mahusiano na mwigizaji Michael Jordan.
Akifanya mahojiano kupitia kipindi cha Ellen show Steve Harvey amesema kuwa mkwe wake ambaye ni Michael Jordan ni kijana mstaraabu sana kwani anajitahidi kuwa karibu na wakwe zake na hata wamefanikiwa kusheherekea sikukuu mbili za krisimasi kwa Pamoja vilevile bwana Harvey ameongeza kuwa Michael ni kijana mtoaji sana kwahiyo anafurahi kuwa sehemu ya familia yake lakini kama akizingua basi atampiga.
Amesema steve ambaye pia alisisitiza kuwa kuna wakati anashindwa kuwa huru kutokana na picha zao wanazoweka katika mitandao ya kijamii.