Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kwa miezi mitatu kipindi cha Efatha Ministry kinachorushwa kupitia kituo cha televisheni cha Star TV, kwa kukiuka kanuni za maudhui ya Utangazaji za mwaka 2018. Uamuzi huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Abby Gunze kwa maelezo kwamba, kipindi hicho kinachorushwa mbashara na Mchungaji Josephat Mwingira kilitumia lugha ya matusi dhidi ya mamlaka ya juu ya nchi.