Kiungo mkongwe wa Real Madrid Luka Modric atasalia katika klabu hiyo kwa msimu mwingine baada ya kuongeza mkataba wake hadi Juni 2024, timu hiyo ya Uhispania ilisema Jumatatu.
Modric, 37, anasalia kuwa mchezaji muhimu wa Madrid na aliamua kusalia licha ya kuwindwa na Saudi Arabia, wakitaka kumsajili mwishoni mwa mkataba wake wa awali, ambao unamalizika mwezi huu.