TFF yahairisha hafla ya tuzo za msimu 2024/2025

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuahirishwa kwa hafla ya utoaji wa tuzo za msimu wa 2024/2025, ambayo awali ilipangwa kufanyika tarehe 5 Desemba  mwaka huu.

TFF imeeleza kuwa uamuzi huo umetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, na kwamba tarehe mpya ya kufanyika kwa hafla hiyo itatangazwa mara baada ya maandalizi kukamilika.

Shirikisho hilo pia limewahakikishia wadau wa soka, klabu, wachezaji na mashabiki kwamba litatoa taarifa rasmi kuhusu utaratibu na ratiba mpya pindi mambo yatakapokuwa tayari.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii