Katika mazungumzo hayo, Macron anatarajiwa kumshawishi Xi kutumia ushawishi wake kwa Urusi, ili kusaidia kufanikisha mpango wa usitishaji wa mapigano, hasa ikizingatiwa kuwa vita hivyo sasa vinaingia msimu wa baridi kwa mara ya nne tangu kuanza kwake mwaka 2022.
Ziara hiyo ya Macron, ya nne tangu 2017, pia inajumuisha kikao na Waziri Mkuu wa China Li Qiang kabla ya kuelekea Chengdu.
Macron amekuwa mstari wa mbele kuihimiza China kuchukua msimamo wa wazi zaidi kuhusu vita hivyo, kufuatia ziara ya hivi karibuni ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky jijini Paris, ambapo aliitaka Ulaya kuendelea kuiunga mkono Kyiv.
China, licha ya kutoa wito wa amani na kuheshimu mipaka ya mataifa, haijawahi kulaani moja kwa moja uvamizi wa Urusi, jambo linaloendelea kuibua maswali kuhusu nafasi yake katika juhudi za kidiplomasia kutatua mzozo huo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime