Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza fursa kwa wamiliki wa mabasi kuwasilisha maombi ya leseni za muda mfupi ili kuongeza huduma za usafiri wa abiria kwenye njia zenye uhitaji mkubwa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Salum Pazzy, leseni hizo zinatolewa kuanzia Desemba 3.
Amesema zinatolewa kwa basi lenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 40 au liwe na leseni ya basi maalum ya kundi.
Kadhalika, amesema basi hilo linatakiwa liwe limeunganishwa kwenye mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari(VTS), lenye bima hai, lenye hati ya uchaguzi kutoka Jeshi la Polisi(VIR) na lenye leseni hai ya LATRA.
Pia, vigezo vingine ni dereva awe ametambuliwa kitufe cha utambuzi(i-button) kilichosajiliwa na LATRA na ambalo limeunganishwa mfumo wa Tiketi Mtandao.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime