Rais Samia afanya mazungumzo na Naibu Mwenyekiti wa Biashara Jumuiya ya Madola

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara wa Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam jana Desemba 02, 2025.

Rais Dkt. Samia pamoja na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Lord Hugo Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza walijadiliana masuala ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira.

Aidha, Lord Swire ameomba Tanzania kuwa mshirika wa kimkakati ili kuchochea wawekezaji wengi kutoka washirika wa Jumuiya hiyo ya Madola.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii