Mbunge Azza awasihi wananchi kulima mazao yanaostahimili ukame

Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad, amewasihi wananchi kulima mazao ambayo yanastahimili ukame kutokana na hali ya hewa kutokuwa nzuri,ambayo inaonyesha kutakuwa na mvua chache.

Amebainisha hayo wakati akitoa salamu kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, la kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu Mwenyekiti na viongozi wa Kamati za kudumu za Halmashauri hiyo.

Amesema hali ya hewa siyo nzuri ambapo kwa kipindi hiki mvua zingekuwa zinanyesha, lakini hadi sasa mvua hazitabiriki,  na kuwasishi wananchi kwamba, walime mazao ambayo yanastahimili ukame ili wapate mavuno.

“Nawaomba Madiwani, mhamasishe wananchi katika maeneo yenu, walime mazao ambayo yanastahimili ukame hali ya hewa inaashiria kupungua kwa mvua msimu huu,”amesema Azza.

Amewasihi pia Wananchi wapande Miti kwa wingi na kuitunza,ili kupata mvua na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Katika hatua nyingine, amewaomba Watanzania kuendelea kulinda Amani ya nchi na wasikubali kuichezea.

Aidha,kwenye kikao hicho Madiwani walimchangua Seth Msangwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Joseph Buyugu Makamu wake.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii