Vikosi viwili vyenye kiwango bora zaidi barani Ulaya vitachuana usiku wa kesho jumatano tarehe 26 kwenye Ligi ya Mabingwa Ndani ya uwanja wa Emirates, London.
The Gunners, ambao wametoka kuisambaratisha Tottenham katika Derby ya Kaskazini London, wako kileleni mwa Ligi ya uingereza kwa alama saba na wanaonekana kuwa wawaniaji wakuu wa kutwaa taji msimu huu.
Kwa upande mwingine, Bayern wamerudi katika ubabe wao wa Bundesliga na wameshinda mechi zote isipokuwa moja katika mashindano yote, wakipoteza pointi pekee ugenini dhidi ya Union Berlin kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa ya Novemba.
Bayern watakosa huduma ya Luis Diaz, aliyepewa marufuku ya mechi tatu baada ya kutolewa nje dhidi ya PSG. Mwanasoka aliyepitia akademi ya Arsenal, Serge Gnabry, anaweza kurejea Emirates kuchukua nafasi ya Mkolombia huyo, endapo atapona tatizo lake la goti kwa wakati.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime