Msanii wa muziki wa bongo fleva kutoka nchini Tanzania ambaye pia anafanya vizuri kwa sasa na ep yake ya MMI,Foby ambaye ameachia video ya moja ya wimbo wake ambayo inapatikana katika ep yake amefunguka kuhusu kilichotokea miezi kadhaa iliyopita kufuatia kutokupata sapoti kutoka kwa wasanii wenzake na kupelekea kuonyesha screenshot za baadhi ya wasanii ambao alikuwa akisapoti kazi zao mpya.
Foby amesema kuwa yeye amezaliwa kusapoti akipiga stori kupitia kipindi cha hitzone ndani ya jembe fm amesema:- “Mimi nimezaliwa kusapoti watu wengine,kwahiyo kitendo cha mimi kuweka screen shot ilikuwa tu ni kuonyesha kuwa huwa na sapoti wenzangu na sitaacha ilimradi mtu akafanya kitu kziuri hata kama hawasapoti cha kwangu mimi nitaendelea kusapoti”
Alisema foby ambaye pia anaamini mwaka huu atafanya makubwa Zaidi kwaajili ya mashabiki zake .