Maelfu ya watu waliandamana jana nchini Ujerumani kupinga vizuizi vya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona na chanjo za lazima huku makundi madogo yakifanya maandamano kinzani
Polisi inasema zaidi ya watu 7,500 walijitokeza mjini Dusseldorf ijapokuwa ni watu 3,500 pekee waliotarajiwa.Watu wengine 2,300 waliandamana katika eneo la Regensburg huku maandamano kinzani yakijaribu kuyavunja maandamano hayo.
Waandamanaji watatu wa maandamano kinzani waliwekwa chini ya ulinzi huku mwengine akikamatwa kwa kuwatusi na kuwashambulia maafisa wa polisi.Katika jimbo la Stuttgart, waandamanaji walisimama nje ya jengo la shirika la utangazaji la umma Südwestrundfunk (SWR) kulikosoa kwa utangazaji wake kuhusu janga la corona.