Kuanzia Februari Nchini Austria, Chanjo kwa Watu wazima itakuwa ni lazima na wote ambao hawajachanjwa watapokea wito wa kuchomwa sindano ya kwanza. Wale ambao hawatajitokeza watatozwa faini baada ya kukumbushwa
Sheria iliyowekwa inatoa hadi faini nne kwa kila Mtu ambapo Polisi watapewa uwezo wa kufanya ukaguzi kwenye Barabara Kuu. Sheria hiyo imepangwa kutumika hadi Januari 31, 2024
Serikali ya Austria inatetea hatua hii kutokana na idadi kubwa ya Wagonjwa katika Hospitali mbalimbali kutokana na maambukizi ya kirusi kipya cha ya Omicron