SERIKALI YASISITIZA KUENDELEA KUSIMAMIA HAKI ZA WATUMISHI.

erikali imesema, zaidi ya Watumishi wa Umma 180,000 wamepandishwa madaraja ambapo Wilaya ya Nkasi iliyopo mkoani Rukwa imenufaika na promosheni kwa watumishi wake 837 kupandishwa madaraja huku watumishi zaidi ya 40 wakibadilishiwa kada zao za utumishi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amatoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambapo pia amesisitiza viongozi wa kiserikali na kisiasa kuacha tabia ya kuwadhalilisha watumishi wa umma pindi wanapokosea.

Ndejembi amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imejikita katika kuwaboreshea maisha watumishi wa umma huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu kazini.

Amesema kuwa Ofisi ya Rais Utumishi itaendelea kutetea haki za watumishi wa umma usiku na mchana na kwamba hakuna haki ya mtumishi yeyote itakayopotea iwe ni kulipwa malimbikizo ya mishahara, kupandishwa madaraja au kubadilishiwa kada.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii