Mwanamitindo na msanii maarufu Bongo, Hamisa Mobetto amekana madai kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Rapa wa Marekani Rick Ross.
Akizungumza katika mahojiano na runinga ya NTV nchini Kenya , Msanii huyo ambaye pia ni mfanyabishara amethibitisha kwamba yeye ni rafiki wa karibu wa mwanamuziki huyo wa Marekani kwa jina William Leonard Roberts II.
“Sisi ni kama familia kubwa na tumefanya vitu pamoja ambavyo nitavizindua hivi karibuni’’, alisema.
Alizungumza wakati wa ziara yake nchini Kenya ambapo anahusika na kazi za hisani katika eneo la Kayole mjini Nairobi.
Hamisa amesema kwamba kwasasa anajaribu kujenga nembo yake na kujitengezea fedha zaidi.
Awali , picha na video za wawili hao wakiwa pamoja ziliwawacha vinywa wazi wapenzi wa mitandao ya kijamii Afrika mashariki huku wote wakikataa kuelezea bayana uhusiano wao.