ALKIA wa muziki wa Bongo Fleva Afrika Mashariki, Nandy The African Princess ameendelea kutrendi na tetesi za kuwa mjamzito kwa wiki kadhaa sasa.
Inasemekana kuwa, Nandy au Nandera alionekana tofauti alipokuwa akizindua lipstick zake za Shushi ambapo baadhi ya watu walidai kwamba ameanza kuonesha dalili za kuwa mjamzito ikiwemo mabadiliko usoni na kuchomoza kwa kitumbo.
Kwa upande wake Nandy amekuwa akiwataka watu kuwa wapole kwani kuna mambo makubwa yanakuja kutoka kwake.
Akijibu swali la kuwa mjamzito, mara kadhaa Nandy ambaye ni mchumba wa msanii Nenga amekiri kuhitaji mtoto mtoto.